Waliopenya Kujiunga Kidato cha Tano Hadharani
Dar es Salaam. Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amesema jumla ya wanafunzi 153,219 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu na elimu ya ufundi kwa mwaka 2022. Kati ya hao, wanafunzi wa 90,825 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mpya 22 za Serikali. Huku akibainisha kuwa kati yao wenye mahitaji maalumu 481. “Wanafunzi 41,401 wakiwemo wasichana 17,390 watajiunga kusoma tahususi za sayansina hisabati. Huku wanafunzi 47,133 wakiwemo wasichana 25,508 watajiunga kusoma tahasusi za masomo ya Sanaa, lugha na biashara,” amesema Bashungwa. Waziri huyo ameeleza hayo leo Alhamisi Mei 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na elimu ya ufundi, akisema wanafunzi hao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu wametoka katika shule za Serikali na binafsi. Bashungwa amefafanua kuwa kati ya wanafunzi 153,219 wasichana 67,751 na wavulana 85,678 sawa na asil...